Banner Banner Right 
Mwanzo | Chumba | Wasiliana nasi | Barua Pepe | Viunga | Ingia
   English | Kiswahili

Bonyeza hapa kuangalia matokeo ya semesta ya kwanza Desemba 2007

CHUO CHA SANAA BAGAMOYO ni taasisi hai yenye ubunifu na uvumbuzi wa kutoa mafunzo, utaalam, na kufanya utafiti katika kiwango cha hali ya juu katika sanaa. Lengo letu ni kuzalisha wasanii wataalam , mameneja wa sanaa , bidh aa na huduma za sanaa katika kiwango cha hali ya juu. Tunajali mafunzo yanayomlenga mwanafunzi na ubora wa hali ya juu kitaaluma. Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambacho kilianzishwa mwaka 1981 ni moja ya taasisi chache sana zinazotoa mafunzo ya sanaa kinadharia na kivitendo katika Afrika. Chuo kimejengwa katika mandhari ya kuvutia ufukweni mwa bahari ya Hindi kilometa 72 kaskazini ya jiji la Dar es Salaam.

Tunatoa mafunzo ya miaka mitatu kwa kiwango cha Diploma yenye ithibati ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi. Masomo makuu ni uchezaji na upigaji NGOMA , TAMTHILIYA , SANAA ZA UFUNDI , MUZIKI na UFUNDI WA JUKWAA .Masomo ya lazima kwa wanachuo wote ni MBINU ZA MAWASILIANO , UKUZAJI UONGOZI WA SANAA , SARAKASI , MBINU ZA UTAFITI , na MAFUNZO YA KOMPYUTA .Aidha, tunatoa kozi fupi katika masomo hayo kati ya miezi mitatu(3) hadi miezi tisa(9) . Mafunzo yetu hutolewa kwa wanafunzi wa Kitanzania na Kigeni

Hili ni tolea la kwanza la tovuti ya chuo chetu. Mipango ya maendeleo ya baadaye itahusisha kurasa binafsi kwa wafanyakazi na wanachuo, itaonyesha picha za matamasha ya Sanaa Bagamoyo, Kongamano, fomu za maombi na kadhalika.

Karibu Tanzania! Karibu Chuo cha Sanaa Bagamoyo!

Juma A. Bakari
Mkuu wa Chuo

Juu
 © Chuo Cha Sanaa Bagamoyo